Serikali kupitia Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, imefanikisha mchakato wa Ajira na kuwapangia vituo vya kazi jumla ya waombaji 55,162.

Akizungumza na Waandishi wa habari Waziri wa Nchi, Ofisi Ya Rais, Menejimenti Ya Utumishi Wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene Wakati akitoa taarifa Kuhusu Mafanikio ya Miaka minne ya Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema waombaji kazi waliopangiwa vituo vya kazi waliongezeka kutoka 7,659 mwaka 2020 hadi 20,158 mwaka 2024, sawa na ongezeko la asilimia 163.19.

Hata hivyo amesema Serikali kupitia Sekretarieti ya Ajira imeendelea kuimarisha na kuboresha utendaji kazi wa Taasisi kwa kutumia mifumo ya TEHAMA ambapo hadi mwaka 2024 Taasisi imefanikiwa kuwa na mifumo sita (6) ambayo ni Portal ya kuajiri, Maombi ya rununu ya portal ya Kuajiri, Dawati la usaidizi, Kanzidata ya Maswali ya Usaili (Questions Databank System – QBS), na Mfumo wa Kupima Uelewa na Ufahamu wa Wasailiwa kwa njia ya mtandao.

Amesema mifumo hiyo imesaidia kuwapunguzia waombaji kazi gharama zinazohusiana na michakato ya Ajira kwa kuwa usaili wa kuandika/mchujo hufanyika kwa njia ya kielektroniki kwenye vituo vilivyo karibu na maeneo wanayotoka.

Aidha, pia imepunguza gharama za kudurufu maswali ya usaili, usahihishaji wa maswali na uhakiki wa maswali kwa kuwa mfumo hufanya kazi zote na Kupunguza siku za kuendesha michakato ya ajira kutoka siku zaidi ya 120 hadi siku pungufu ya 50.

Hata hivyo, amesema Hadi kufikia Desemba, 2024, jumla ya miradi 27,863 ya kutoa ajira za muda kwa walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini imetekelezwa ambapo jumla ya Kaya za Walengwa 662,000 zimelipwa jumla ya shilingi bilioni 213.8.

Ameongezea kwa kusema licha ya kuongeza kipato, walengwa pia wameweza kupata ujuzi wa utekelezaji wa miradi hiyo unaoweza kutumika katika shughuli za kukuza uchumi wa kaya na kuongeza kipato, Miradi hiyo imenufaisha sekta za kilimo, barabara, misitu, maji na mazingira.

Habari kuu kwenye Magazeti yaleo Aprili 21, 2025
Kikwete ahitimisha ziara kwa kukutana na Captain Ibrahim Traore