Johansen Buberwa – Kagera.

Wananchi wa Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera, wamejitokeza kwa wingi kumuaga mdau Mazingira na Maendeleo Mkoani humo, Mtanzaniaa Julianus Bahati Kimodoi ailiyekuwa akiishi Nchini Marekani, ambaye enzi za uhai wake alikuwa mhamasishaji mkubwa wa shughuli mbalimbali za kimaendeleo.

Akiongoza ibada ya Mazishi ya Mdau huyo, Padre Samweli Mchunguzi Paroko wa Parokia ya Bukoba ambaye pia ni Makamu wa Askofu wa jimbo hilo amesema jamii inatakiwa kubadilika na kuwa hofu ya MUNGU na wakawe watu wa kutenda haki kwa kusimamia ukweli kama alivyo kuwa akifanya marehemu Kimodoi wakati wa uhai wake.

Padre Samweli Mchunguzi, Paroko wa Parokia ya Bukoba.

amesema, “tuwe na hofu ya MUNGU tuwe watu wa haki tuwe watu wa kusimamia ukweli tusiutwazwe utu wetu tusisaliti imani zetu maana hakuna imani inayosema tuwafanyie wengine fujo,”

“”Maana katika nyumba zetu za imani tunafundishwa kupendana tusisahau kwa maana sisi ni binadamu tuzingatie upya amri za Mungu kanisa na wajibu zetu tutoke hapa tukiwa tumedhamilia kuwa watu kweli kwa kuishi kwa upendo tusaidiane kwa ndugu yetu ailiyeondoka kunamema ameyatenda,” aliongeza Padre Muchunguzi.

Naye Mkuu wa Wilaya Bukoba, Erasto Sima amesema itamuenzi Kimodai kwa mema aliyoyaacha, huku Mbunge  wa viti Maalumu Mkoa wa Kagera, Oliver Semguruka akisema jamii imempoteza shujaa.

“Kwa imani naamini kwa vita alivyo vipigana hapa duniani atakuwa kifuani mwa Ibramu kwa maana Kimodoi alipenda sana maendeleo na ninamuombea msamaha kwa wale aliowakosea, ili apumzike kwa amani maana kama binadamu sote ni njia moja.

Mkuu wa Wilaya Bukoba, Erasto Sima.

Awali, Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Mkoa wa Kagera, Hamim Mohamud akizungumza kwa niaba ya chama alisema Kimodoi aliwaunganisha Wanakagera wa ndani na nje ya nchi walijiona kama wapo ndani Bukoba.

“Na kingine aliweza kuchechemua miradi ya maendeleo kwa kugusa ilani ya ccm hasa kwa upande wa mazingira kwa kupanada miti ya Pamtree na uzio wa shule ya sekobdari Bukoba Sondari ambavyo ni vielelezo vitabaki kwenye picha na nyoyo za watu na waliobaki tunajiliza tutaacha alama gani kwenye jamii inayowazunguka,” aliongeza.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa Kagera, Hajjat Fatma Mwassa akizungumza kwa njia ya simu amesema Kimodoi alikuwa mdau mkubwa wa kuchagiza shughuli mbalimbali za kimaendeleo ndani ya mkoa huo na mkoa huo umebaki na alama.

Kipindi cha uhai wake, Julianus Bahati Kimodoi alihamasisha utunzaji wa Mazingira kwa kupanda miti Manispaa ya Bukoba na ujenzi wa uzio katika bweni la wasichana Shule ya Sekondari Bukoba.

Mbunge Viti maalumu Mkoa Kagera, Oliver Semguruka.

Pia, alihamasisha ujenzi wa Bweni la Wasichana Omwani pamoja na huduma mbalimbali za kijamii kwa wagonjwa akiwa ni mtoto wa kwanza kati ya saba kwenye familia yeye akiwa mzaliwa wa mwaka 1973 huko Bukoba na alifariki 2025 alikuwa akiishi Jimbo la Texas Nchini Marekani.

Katibu Siasa na Uenezi CCM – Mkoa Kagera, 

Hamimu Mohamudu.

Mchango wa Sekta ya Madini katika pato la Taifa wafikia asilimia 10.1
Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Aprili 23, 2024