Maadhimisho ya siku ya Usalama Mahala pa kazi Duniani tarehe 28, April mwaka huu, kufanyika Mkoani Singida Kitaifa.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Waziri Wa Nchi, Ofisi Ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Ridhiwani Kikwete ambapo amesema Maadhimisho hayo kwa mwaka huu yamebeba kauli mbiu isemayo “Nafasi ya Akili Mnemba na Teknolojia za Kidijitali katika Mapinduzi ya Usalama na Afya Kazini.

“Kauli Mbiu ya mwaka huu imelenga kuhamasisha na kuwakumbusha waajiri kuanza kujiandaa kutumia Akili Mnemba katika uzalisha na utoaji huduma bora”, amesema

“Matumizi ya Akili Bandia (AI) na Teknolojia ya Kidijitali kazini ni eneo ambalo linabadilisha kwa kasi namna tunavyofanya kazi, kuwasiliana na hata kulinda usalama wetu kazini”. Amesema Ridhiwani

Amesema Teknolojia hiyo imeleta mabadiliko chanya mengi na baadhi ya mabadiliko hayo ni kama mashine na mifumo ya inayotumia akili mnemba kufanya kazi haraka, kwa usahihi mkubwa na bila kuchoka, Roboti na mifumo ya kidijitali sasa hufanya kazi hatarishi ambazo zamani zilifanywa na binadamu, hivyo kuepusha wafanyakazi na ajali, Sensori za kisasa husaidia kugundua hatari kama vile gesi hatari au moto mapema zaidi kuliko binadamu na Teknolojia ya mtandaoni huwezesha wafanyakazi kujifunza bila kuondoka kazini au kusafiri kwenda kufanya mafunzo.

“Pamoja na Faida za matumizi ya Akili Mnemba, Hata hivyo kuna changamoto kadhaa zinazoweza kujitokeza wakati wa matumizi ya mashine zinazotumia akili mnemba”,

“Baadhi ya changamoto hizo ni kama vile Mashine na roboti kuchukua nafasi ya wafanyakazi kumesababisha hofu ya ukosefu wa ajira, hasa kwa kazi zisizohitaji ujuzi mkubwa, matumizi ya teknolojia ambayo bado haijaelewaka vizuri kwa wafanyakazi inaweza kusababisha tatizo la kisaikolojia, ikitokea hitilafu za kimtandao au mfumo, shughuli nyingi zinaweza kuathirika, na Mfumo wa kidijitali unaweza kuvamiwa, na taarifa za wafanyakazi au kampuni kuvuja”. Amesema Ridhiwani

Vilevile amesema ni vizuri kutambua kuwa matumizi ya akili mnemba na teknolojia hayamaanishi kupotea kwa ajira zote, bali yanaleta mabadiliko katika aina ya ajira.

“Matumizi ya teknolojia hizo yataleta ongezeko la mahitaji ya wataalamu wa teknolojia, mafundi wa mitambo ya kisasa, na wasimamizi wa taarifa na mifumo ya akili mnemba”,

“Hata hivyo, hii inahitaji mipango ya mafunzo na kujenga uwezo mpya kwa wafanyakazi wa sasa na wa baadaye”. Amesema Ridhiwani.

Miradi iliyosimamiwa vizuri ilete Matokeo kwa Wananchi - Mbano
Rais Samia aisapoti Simba, agharamia malazi, usafiri