Serikali imewasilisha vipaumbele 5 vya Ofisi ya Msajili wa Hazina (OMH) kwa mwaka wa fedha 2025/26, likiwa ni pamoja na utekelezaji wa Mpango wa Muda Mrefu wa miaka 25 (2025/26–2049/50) kwa usimamizi bora wa mali za umma.
Prof. Kitila Mkumbo amesema, OMH itaendelea kufanya tathmini ya mali zilizobinafsishwa, kuimarisha TEHAMA kwa ukusanyaji wa mapato yasiyo ya kodi kupitia dashboard mpya, na kusimamia kwa ufanisi taasisi na mashirika ya umma kwa kutumia miongozo mahsusi ya bodi.
Aidha, OMH inalenga kukusanya Sh 1.56 trilioni kutoka vyanzo visivyo vya kodi — ongezeko kubwa kutoka Sh1.113 trilioni ya mwaka 2024/25.
Hadi Machi 2025, Sh664.53 bilioni (60%) zilikusanywa, na maboresho ya mifumo kama PlanRep, ERMS, e-Watumishi na MUSE yameongeza uwazi na uwajibikaji.