Naibu Waziri Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Zainab Katimba amewaelekeza wakurugenzi wa Mamlaka za serikali za mitaa kutengeneza mchanganuo na kubaini watumishi wangapi wanadai malimbikizo ya mishahara na yasiyo yamishahara na kuyawasilisha Utumishi kuhakikiwa na kupekwa hazina kwaajili ya malipo.
Ameyatoa maelekezo hayo bungeni Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Segerea, Bonnah Kamoli kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Mohamed Mchengerwa aliyetaka kujua serikali inampango gani wa kulipa malimbikizo ya mishahara na marupurupu ya Walimu.

Akijibu hilo Katimba amesema, “naomba nitoe msisitizo huo na jana kwenye bajeti ya wizara ya utumishi maelekezo hayo yalitolewa na wizara hiyo na mpaka itakapo fika tarehe 31 Mei wakurugenzi wote wawe wamewasilisha majina hayo ya watumishi hao ambao wanadai malipo yao.”
Kuhusu mazingira bora ya Walimu, Katimba amesema serikali inaendelea kujenga nyumba za walimu ili walimu wapate mazingira mazuri ya kuishi na kufanyakazi kwa ufanisi.