Mkuu wa Wilaya ya Makete, Kissa Kasongwa amewataka Watendaji wa Kata kuwa wabunifu katika Utekelezaji wa afua za Lishe kwenye maeneo yao wanayoyasimamia.
Ametoa Rai hiyo wakati wa Kikao cha upokeaji wa Taarifa za utekelezaji wa afua za Lishe, kwa Robo ya tatu, kuanzia mwezi wa kwanza hadi wa tatu, kwa mwaka wa Fedha wa 2024/2025.

Aidha, ameipongeza kazi nzuri inayofanywa na Afisa Lishe wa Halmashauri ya Wilaya ya Makete, Jackline Nanauka pamoja na Halmashauri nzima kwa ujumla kwa utekelezaji mzuri wa afua za Lishe.