Mwili wa mtu mmoja jinsia ya kiume ambaye jina lake bado halijatambuliwa umekutwa ukielea katika mto Misunkumilo uliopo Wilaya ya Mpanda mkoani Katavi.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Katavi, Emannuel Ndoshi amedai kuwa mwili huo umekutwa na majeraha na kudai kuwa umesafirishwa na maji kutoka sehemu ambayo bado haijajulikana.
Wakazi wa maeneo hayo wamesema, waliuona mwili huo ambao hata hivyo wanadai hawakuutambua ndipo walipotoa taarifa kwa jeshi la zimamoto na uokoaji.