Na johansen Buberwa – Kagera.
Zaidi ya Kaya 54 kwenye vitongoji vitano ndani ya vijiji viwili tarafa ya Bugabo Halmashari ya Bukoba Mkoani Kagera nyumba zao zimeathiriwa na Mvua Kubwa iliyoambatana na upepo Mkali uliodumu kwa muda wa saa moja na nakupeleke familia 18 kukosa makazi huku migomba 4198 kuharibika.
Akizungumzia tukio hilo, Mkuu wa Wilaya Bukoba, Erasto Sima hii leo mei 3, 2025 amesema Kamati ya Usalama ya wilaya hiyo ileweza kwanda kwenye vijiji hivyo mei 02 mwaka huu na kujionea kwa namna ya athari ilivyoweza kuvikumba vijiji hivyo na tayari Serikali ipo kwenye mchakato wa kuratibu vitongoji vyote namna wa namna ya kuwasaidia wanachia hao ambao wamepata madhara ya kuharibikiwa mali zao.

Mkuu wa Wilaya Bukoba, Erasto Sima akiwa eneo la tukio kuwatembelea wahanga.
“Kwa sasa familia zile amabazo zimeathiriwa na makazi wanakijiji wenzao tunaomba wanaendelea kuwasaidia wananchi waliothiriwa na mvua za upepo katika kipindi hiki ambacho Serikali inaendelea kulifanyia ufumbuzi jambo hilo na wananchi tuendelee kujenga nyumba ambazo ni imara,” amesema Sima.
Awali, akisoma taarifa ya athari zilozo vikumba vijiji hivyo, Mtendaji wa Kata ya Kishanje, Mpandabilima Esk amesema Kijiji Kishanje vitongoji vilivyoweza kuathiriwa vitongoji viwili ambavyo ni Mwijambele Bugashani na Kijiji Bumai viliathiriwa vitongoji vitatu ni Buhinda Kanyamayenje pamoja na Kandago na nyumba 19 n miti 41.

“Na uharibifu mwingine wa mazao ni Magimbi Mihogo na Vanila ilikuwa tarehe 30 mwezi April mwaka 2025 majira ya saa mbili na nusu asubuhi mpaka saa tatu na nusu asubuhi”amesema Mpandabilima.
Kwa upande wake Katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya Bukoba Vijijini Jesca Ndamukama amesema wanatoa pole kwa wanchi hao ambao wamepata athari za mvua hizo ndani kipindi hiki amabcho ni kigumu kwa upande wao na kuwaomba waendelee kuwa na subira wakati jambo hilo likiwa linashughulikiwa.