Waziri wa Madini, Anthony Mavunde amezindua mradi wa uchimbaji Madini ya dhahabu kwa vijana, wanawake na wenye ulemavu kwa kutoa leseni za uchimbaji mdogo wa madini ikiwa ni utekelezaji wa Programu ya Mining For a Brighter Tomorrow (MBT).
Amezindua mradi huo leo Mei 03, 2025 katika viwanja vya shule ya sekondari Ingwe vilivyopo katika eneo la Nyamongo wilayani Tarime Mkoa wa Mara ambapo ametoa leseni 48 za uchimbaji mdogo wa madini kwa wanufaika zaidi ya 2000 vijana, wanawake na wenye nahitaji maalumu.

Akizungumza katika hafla hiyo amesema, Wizara ya Madini imekamilisha maandalizi ya Programu ya MBT ambayo itatekelezwa katika kipindi cha miaka mitano kuanzia mwaka 2025 hadi 2030.
Programu hiyo ni ya kimageuzi katika Sekta ya Madini ambayo imeanzishwa kwa ajili ya kushughulikia changamoto na kuboresha fursa kwa wanawake, vijana na watu wenye mahitaji maalum ili kuongeza ushiriki wa makundi hayo katika mnyororo wa thamani wa madini.

“Naomba nichukue fursa hii kumpongeza Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye yeye alitupa maelekezo kuhakikisha vijana, wanawake na wenye mahitaji maalumu wanashiriki kikamilifu katika shughuli za madini.
hususan katika eneo la Sekta ya Madini ambapo amesema juhudi za Waziri huyo zinaonekana kwa vitendo na kuomba vijana hao wajengewe uwezo ili waweze kuchimba kwa tija.
Sambamba na hayo, Kanali Mtambi amemuomba Waziri Mavunde kutoishia kwenye utoaji wa leseni pekee bali pia kuliangalia suala la msaada wa kiufundi pamoja na mitaji ili kuwawezesha wachimbaji hao kufanya kazi kwa tija.

Naye, Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wachimbaji Wadogo Tanzania (FEMATA), John Bina amempongeza Waziri Mavunde kwa kuzindua mradi huo na kuwataka vijana, wanawake na wenye mahitaji maalumu kufanya kazi kwa kushirikiana na kuepuka migogoro isiyo ya lazima.