Johansen Buberwa – Kagera.
Jumla ya matukio 74 ya moto na maokozi yameripotiwa mkoani Kagera kwa kipindi cha miezi 10, huku vikoba na uzembe vikitajwa kuwa visababishi vya ajali hizo.
Akizungumza wakati wa kilele cha maadhimisho ya wiki ya Zimamoto Duniani ambayo huadhimishwa Mei 4 kila mwaka, Mrakibu wa Jeshi la zimamoto na uokoaji, Joseph Ngonyani amesema kwa kipindi cha Julai 2024 hadi Mei 2025 yameripotiwa matukio 62 yakihusishwa na moto 12 ni maokozi Mkoani humo.
Amesema, “yawezekana kunamtu anahifadhi kibubu kinafedha mwisho wa siku unakuta zile fedha amezitumia wanakikundi au wanachama wanapohitaji zile pesa zao kwakuwa hana anaweza akachoma moto katika hilo jengo ambalo limehifadhi ile pesa ili ionekane zile pesa zimeteketea lakini unakuta ilepesa ameitumia kwa matumizi yake binafsi.”
Aidha, Ngonyani ameitaka jamii kuendelea kutoa Ushirikiano kwa jeshi hilo kwa wakati ili jeshi liweze kufika eneo la tukio kwa wakati na kudhibiti moto ili kutosababisha madhara makubwa zaidi pamoja na wahakikishe wanatunza miundombinu ya maji kwa ajiri ya kuzima moto iliyo kwenye maeneo yao.
Baadhi ya wananchi walioshiriki maadhimisho hayo akiwemo Cletus Mutakyawa na Joseph Maduhu wamesema matukio ya moto yamepungua tofauti na kipindi cha nyuma kwani Wananchi wamepewa elimu ambayo imesewaidia kwa Baadhi yao kutoa taarifa kwa wakati.