Serikali inatarajia kuzindua Kampeni ya Chanjo ya Mifugo Kitaifa kati ya mwezi Mei hadi Juni, 2025 ambapo jumla ya dozi 19,099,100 za chanjo ya Homa ya Mapafu ya Ngombe (CBPP) zimenunuliwa na zinatarajia kuchanja jumla ya ng’ombe 19,099,100.

Akizungumza Leo Jijini Dodoma Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Ashatu Kijaji wakati akitoa taarifa ya Mafanikio Wizaya hiyo katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya awamu ya sita ambapo amesema Jumla ya
dozi 17,224,200 za chanjo ya Sotoka ya Mbuzi na Kondoo kwa ajili ya kuchanja
mbuzi na kondoo 17,224,200, na dozi 40,000,000 za Chanjo ya ugonjwa wa
kideri/mdondo (ND), ndui na mafua ya kuku kwa ajili ya kuchanja kuku wa asili
40,000,000.

Amesema Uchanjaji huu, utaiwezesha Tanzania kukidhi masharti ya biashara ya mifugo na mazao yake kulingana na matakwa ya Shirika la Afya ya Wanyama Duniani (WOAH),Shirika la Kilimo na Chakula la Umoja wa Mataifa (FAO), na Shirika la Biashara Duniani (WTO).

Vilevile amesema, Serikali imenunua jumla ya hereni za kidijitali 36,323,300 kwa ajili ya utambuzi wa ng’ombe 19,099,100, Mbuzi na Kondoo 17,224,200 watakaochanjwa.

Amesema Lengo kuu la utambuzi wa mifugo ni Kukidhi matakwa ya soko la kikanda na kimataifa linalohitaji kila mnyama na mazao yake kuwa na alama ya utambuzi, kuwezesha wafugaji kupata mikopo na bima, Kudhibiti wizi wa mifugo, kurahisisha ufuatiliaji na udhibiti wa magonjwa ya wanyama, na kuwezesha Serikali na wadau kuweka mipango ya kuhudumia mifugo kwa kuwa idadi yao inajulikana.

BD yalamba udhamini wa Mil 639.5 wa betPawa
Vitambulisho vya Wazee: Madiwani Mbulu watoa maelekezo