Bunge la Tanzania limepinga uamuzi wa Bunge la Ulaya (EU) kwa kitendo chake cha kuitaka serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuruhusu watetezi wa haki za wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja (ushoga).

Wabunge kadhaa wamesimama bungeni leo kutolea msimamo uamuzi wa Bunge la Ulaya kuhusu haki za wapenzi wa jinsia moja, wakisema Tanzania haiwezi kukubali kuruhusu vitendo hivyo, licha ya kauli iliyotolewa na EU.

Mbunge wa Tarime Vijijini, Mwita Waitara, amesema hoja zao hazina faida kwa nchi, hata kama wamekuwa wakisaidia katika mambo mbalimbali. “Kama hoja yao ni kwamba hawataleta maji, basi tutakunywa hata maji ya kisima,”Alisema Waiitara na kuungwa mkono na wabunge wenzake ndani ya Bunge hilo.

Jana Mei 7, 2025, Bunge la Ulaya lilitoa maazimio sita kuhusu Tanzania, ambapo mbali na agenda ya wapenzi wa jinsia moja, pia waliitaka Mahakama kumuachia Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu anayeshtakiwa kwa makosa ya uchochezi na uhaini.

Maisha: Simulizi iliyoleta fedheha kwa baba na mtoto
Bunge la Ulaya lataka haki kwa Lissu, Waandishi wa Habari