Afarah Suleiman, Babati – Manyara.
Chama cha Mapinduzi Jimbo la Babati Mji mkoani Manyara kimesema hakitakuwa tayari kuwaacha madiwani wa kata hiyo waliosimamia vizuri fedha za miradi ya maendeleo ktk kipindi cha miaka Mitano ya Uwakilishi wao kwa wananchi na kuunga mkono utekelezaji wa ilani ya Chama hicho.
Tamko hilo limetolewa na Mwenyekiti wa Chama hicho, Elizaberth Bombo Malley kwenye Baraza la Robo Mwaka wa fedha 2024/2025 lililofanyika mjini Babati mkoani humo.
Awali akifungua kikao cha Baraza Hilo Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji wa Babati Abdulrahaman Kololi katika hotuba yake amesema licha ya kuwepo kwa changamoto za madeni lakini madiwani hao wamefanikiwa kusimamia utekelezaji wa ilani ikiwa ni pamoja na kusimamia fedha za miradi ya maendeleo kwa wananchi .
Hata hivyo kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya mji wa Babati Simon Mumbe amesema kabla ya kuanza kwa mwakà wa fedha Halmashauri hiyo itakamilosha changamoto zilizopo ikiwa ni pamoja na kuanza miradi ya barabara za kiwango cha lami ili kutekeleza ilani ya Uchaguzi ya 2020/2025.