Baadhi ya viongozi kutoka kwenye Kanda nane za Tanzania Bara za Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), wamesema kuwa wamejivua uanachama wa chama wa hicho kwa sababu ya kupoteza uelekeo na kudai kuwa chama hicho kimegeuka kuwa ni kikundi cha harakati.
Basil Lema Katibu wa Chadema Mkoa wa Kilimanjaro, amesema kuwa Watanzania wamechoka kusikia hadithi ya chama ambacho kilishapanda juu kisiasa na kushuka chini.
Amesema kuwa chama hicho kwa sasa kimetawaliwa na chuki “ndani ya chama chetu uhuru wa kujumuika haupo ukijumuika na Lissu ni sawa lakini ukijumuika na Mbowe wewe ni msaliti.”
Amesema kuwa ndani ya chama hicho hakuna tena uhuru wa kukosoa “Chanzo cha chuki hizi ni aina ya kampeni alizofanya yule bwana mkubwa alishinda uchaguzi alikuwa ana nguvu ya kutumia vyombo vya habari, vijana wadogo wanatukana sasa zile silaha tulitegemea zitumike wakati wa uchaguzi zitarudisha ghalani.”