Upatikanaji na usambazaji wa mbegu bora umefikia tani 79,700.62 sawa na asilimia 99.6 ya lengo la kuzalisha na kuthibitisha tani 80,000 za mbegu dhidi ya mahitaji ya tani 127,650.

Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe ameyasema hayo Bungeni jijini Dodoma, wakati akiwasilisha hotuba kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026 ambapo amesema Kati ya hizo, tani 63,526.54 zimezalishwa nchini na tani 16,174.08 zimeingizwa kutoka nje ya nchi.

Amesema, “kati ya mbegu zilizozalishwa nchini tani 4,510 zimezalishwa na ASA na tani 59,016.54 zimezalishwa na sekta binafsi. ASA imeipatia sekta binafsi mashamba yenye ukubwa wa hekta 5,038 sawa na asilimia 102 ya lengo la hekta 4,914 kwa ajili ya kuzalisha mbegu za mazao ya mahindi, mpunga, alizeti, ngano, maharage na ufuta.”

Bashe amesema tani 700 za mbegu bora za alizeti na tani 500 za mbegu bora za ngano zenye thamani ya Shilingi 17,380,000,000 zimesambazwa kwa wakulima katika maeneo ya uzalishaji kupitia mpango wa ruzuku.

“Tani 9,639.63 za mbegu bora za mahindi zenye thamani ya ruzuku ya Serikali ya Shilingi 10,473,750,000 zimesambazwa kwa wakulima katika maeneo ya uzalishaji kupitia mpango wa ruzuku, Mbegu bora za kahawa tani 9.9 zikiwemo tani 5 za arabika na tani 4.9 za robusta zimezalishwa,” aliongeza Jafo.

“Kati ya hizo, tani 9.2 zimesambazwa kwa wakulima katika maeneo ya uzalishaji na usambazaji unaendelea,” amesema.

Aidha, amesema Marekebisho ya tindikali ya udongo yamefanyika ambapo jumla ya tani 1,100.2 za chokaa mazao zimenunuliwa na kutumika katika mashamba tisa (9) ya mbegu ya Mbozi (hekta 260), Dabaga (hekta 400), Kilimi (hekta 400), Msungura (hekta 100), Mwele (hekta 300), Bugaga (hekta 120), Arusha (hekta 450), Namtumbo (hekta 1,384) na Kilangali (hekta 400). Aidha, marekebisho ya tindikali ya udongo yanaendelea katika shamba la mbegu la Luhafwe (hekta 150).

DC Semindu awakumbusha Wananchi umuhimu wa kulinda amani
Serikali yakamilisha ujenzi Skimu mpya za Magurukenda