Afarah suleiman, Babati-  Manyara.

Mkuu wa Idara ya Kilimo na Mifugo, Mhandisi Agrey Mawole amesema Serikali imeendelea kuboresha mazingira ya Gulio kwa kujenga uzio ili kuzuia mifugo isipotee ,kujenga karo la kuchinjia mifugo,sehemu ya kupakia mifugo kwenye usafiri na kusimika mzani wa kupimia mifugo inapofika kabla ya kuuzwa.

Mahitaji mbalimbali pamoja na mifugo vinapatikana kwa bei nafuu katika Gulio pia ni chanzo kizuri cha mapato ya Halmashauri kupitia ukusanyaji ushuru wa wafanyabiashara .

 

“Kupitia Gulio hili linalofanyika mara mbili kila mwezi limesaidia kuboresha maisha ya familia yangu kwa kuongeza kipato Cha familia, kusomesha watoto, kujenga nyumba bora na kuinuka kiuchumi,” ameeleza Agripina Peter mfanyabiashara.

Juma Mkude Meneja wa Gulio anaeleza kuwa hali ya usalama ni shwari, Wafanyabiashara wanafanya biashara zao kwa amani na utulivu.

BRELA yaweka kambi ya huduma Kliniki ya Biashara Kariakoo
Maisha: Taharuki! Wakuta nywele za binadamu kwenye chakula