Wakala wa Biashara na Leseni (BRELA) imeweka kambi ya kutoa huduma ya Kliniki ya Biashara kwa wafanyabiashara wa Kariakoo.

Kliniki hiyo imelenga kuwahudumia wafanyabiashara wa Kariakoo ili kuweza kuwatatulia changamoto mbalimbali za kiusajili pamoja na zile za Kitehama.

Mbali na utatuzi wa changamoto hizo, pia imetumia kliniki hiyo kuwasaidia wafanyabiashara wa Kariakoo kurasimisha biashara zao kwa kuwasajili Majina ya Biashara, Kampuni, Alama ya Biashara pamoja na Leseni za Biashara.

Pia ukaguzi elimishi utafanyika kwenye maduka ya wafanyabiashara ili kuwapa elimu juu ya umuhimu wa kuwa na Leseni ya Biashara Kundi A hasa kwa wale wanaofanya biashara yenye sura ya Kimataifa.

RC Sendiga aipa kongole Mbulu TC kwa kupata hati safi
Gulio la Gulio la Gendi kuwainua kiuchumi Wakazi wa Babati