Kambi ya kuunda timu ya mkoa Manyara imekamilika ambapo jumla Wanafunzi 120 kutoka Halmashauri zote za Mkoa wa Manyara watakwenda kuwakilisha Mkoa katika mashindano ya UMITASHUMTA Kitaifa yanayotarajiwa kufanyika Mkoani Iringa kuanzia Juni 7, 2025.
Aidha Wanafunzi waliochaguliwa kuendelea kitaifa wanaendelea na Kambi ya mazoezi kwa muda wa siku tatu, ili kujiandaa na mashindano hayo ya kitaifa.
Afisa Elimu Mkoa wa manyara Halfan Omary amewataka wanafunzi ambao hawajachaguliwa kutokata tamaa na pia wajiandae kwa msimu ujao wa mwaka 2026/2027.