Jumla ya Wanafunzi 149,818 wakiwemo wasichana 76,491 na wavulana 73,327 wamechaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano katika Shule 694 za sekondari za Serikali.
Ameyasema hayo leo Jijini Dodoma Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mita (TAMISEMI), Mohamed Mchengerwa wakati akizungumza na Waandishi wa habari kuhusu uchaguzi wa Wanafunzi kujiunga na Kidato cha tano na vyuo vya Elimu ya ufundi Kwa Mwaka 2025 ambapo amesema jumla ya Wanafunzi 141,146 waliofanya Mtihani wa Kidato cha Nne mwaka, 2024,wenye sifa wakiwemo wasichana 72,337 na wavulana 68,809.
Anafunzi hao wamepangwa katika shule za bweni na Wanafunzi 6,944 wakiwemo wasichana 3,353 na wavulana 3,591 wamepangwa katika shule za kutwa.
“Jumla ya wanafunzi laki 214,141 wakiwemo wasichana elfu 97,517 na wavulana laki 116,624 ambao walikuwa na sifa za kuchaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo vya Elimu ya Ufundi ikijumuisha wanafunzi 1,028 wenye mahitaji maalum”, amesema
Amesema Wanafunzi hao wenye sifa wamechaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano katika Shule 694 za sekondari za Serikali ambapo Wanafunzi elfu 1,728 wakiwemo wasichana 801 na wavulana 927 wamepangwa katika shule za sekondari 8 zinazopokea wanafunzi wenye ufaulu wa juu zaidi.
“Wanafunzi 2,875 wakiwemo wasichana 1,057 na wavulana 1,818 wamechaguliwa kujiunga na fani mbalimbali katika Vyuo 04 vya Elimu ya Ufundi, vyuo hivyo ni Chuo cha Ufundi cha Arusha (ATC), Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT), Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST) na Chuo cha Maendeleo ya Maji (WMDI)”, amesema.
“Wanafunzi 2,214 wakiwemo wasichana 1,099 na wavulana 1,115 wamechaguliwa kujiunga na Vyuo vya Afya ngazi ya Stashahada, Wanafunzi 1,609 wakiwemo wasichana 443 na wavulana 1,166 wamechaguliwa kujiunga na Vyuo vya Ualimu kozi za Stashahada na Wanafunzi 57,625 wakiwemo wasichana 18,427 na wavulana 39,198 wamechaguliwa kujiunga na Vyuo vya Kada mbalimbali”. Amesema Mchengerwa
Hata hivyo amesema muula wa kwanza kwa wanafunzi wa Kidato cha Tano utaanza tarehe 08 Julai, 2025.
“Hivyo Wanafunzi wote waliopangwa kujiunga na Kidato cha Tano kwa mwaka, 2025 wanapaswa kuanza kuripoti Shuleni kuanzia tarehe 06 Julai, 2025 na kwamba na Siku ya mwisho ya kuripoti itakuwa tarehe 21 Julai, 2025”