Katika kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Serikali inatarajia kusoma bajeti ya uchaguzi kwa Mara ya kwanza June 12, 2025 Bungeni Jijini Dodoma.
Akizungumza na Waandishi wa habari Msemaji Mkuu wa Serikali na katibu Mkuu Wizara ya habari, sanaa, utamaduni na michezo, Gerson Msigwa Leo Juni 11,2025 Jijini Dodoma ambapo amesema, Bajeti kuu ya Serikali inategemewa kuwasilishwa Juni 12 hivyo kupitia bajeti hiyo na bajeti ya uchaguzi mkuu kwa Mara ya kwanza itasomwa Juni 12, 2025.
“Kubwa kabisa hii ni bajeti yetu ya uchaguzi, kwasababu ndio itakayotoa pesa kwaajili ya kuhudumia uchaguzi wetu unaotarajiwa kufanyika mwaka huu, kikubwa na muhimu kwa Watanzania wote, tunakwenda kuwasilisha bajeti ya uchaguzi kwa pesa zetu wenyewe”, amesema
“Nchi yetu imeanza kugharamikia pesa za uchaguzi kwa kutegemea pesa zetu wenyewe badala ya Fedha za wafadhili, ili ni jambo muhimu la kujivunia sisi Watanzania”. Amesema Msigwa
Hata hivyo ametoa onyo kwa Vijana Wanaotumia vibaya mitandao ya Kijamii kuaswa kuacha mara moja na kutumia mitandao hiyo kujifunza na kujikwamua kiuchumi na kuacha matusi na uchochezi hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu.
“Serikali haitasita kuchukua hatua kali za kisheria kwa watu wote wanaopotosha umma hususani vijana wanaotumia mitandao Kwa njia zisizofaa hasa vijana wa vyuo vikuu kuacha kutumika kuichafua serikali kwa kuandika mambo ambayo yanaigombanisha serikali na wananchi wake”,amesema
“Tumieni mitandao kujielimisha na kama vijana wafanya biashra basi tumieni mitandao hiyo kutangaza biasahra zenu badala ya kufanya vitu ambavyo vinaweza kuwaingiza matatizoni kwani sheria ipo na vyombo vya dola vipo na wengi ambao tumekuwa tukiwakamata wanasema walikuwa hawajui lakini kutokujua siyo sababu ya kuvunja sheria”. Amesem Msigwa