Afarah Suleiman, Mbulu – Manyara.

Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu imefanya Kongamano la vijana na Haydom Nyama Choma Festival, ikiwa na lengo la kuwawezesha vijana na kuwajengea uwezo kwenye masuala mbalimbali ya kiuchumi.

Tamasha hilo ni sehemu ya maandalizi katika kuelekea siku ya Mwenge wa Uhuru Juni 17, 2025 na linafanyika leo hii katika Kata ya Haydom, Juni 13, 2025.

Kongamano hilo lilifunguliwa leo Juni 13 na mkuu wa wilaya ya Mbulu Michael John Semindu ambapo Moja kati ya mambo ambayo vijana wameaswa ni uthubutu, fursa za mikopo kwa vijana, kujiamini na kuanza na walichonacho bila kusubiri kupata mtaji mkubwa.

Aidha,  baada ya kongamano, vijana na wageni waalikwa watapata wasaa wa kula nyama choma ambayo ni sehemu ya kongamano hilo.

Kampeni PIKA SMART inayohamasisha Matumizi Nishati Safi ya Kupikia yazinduliwa
Maisha: Kidole cha binadamu chakutwa ndani ya keki