Mkuu wa Wilaya ya Mbulu mkoani Manyara, Michael Semindu amewataka Wazazi na walezi Wilayani humo kuwa mstari wa mbele kuzingatia haki na malezi ya watoto wao

Semindu ametoa Rai Leo juni 16/2025 alipozungumza na Wananchi katika maadhimisho ya siku ya kimataifa ya mtoto wa afrika ,ambo kiwilaya yamefanyika katika Kata ya Ayamaami wilayani humo.

” Wazazi na jamii nzima tunalo jukumu la kushiriki kikamilifu katika suala zima la malezi na makuzi ya watoto kwa kuzingatia haki na Usawa,” alisema Semindu.

Sambamba na hayo Semindu amesisitiza kuendelea kuwalea watoto kwa kuzingatia maadili ya kiafrika ili kujenga kizazi bora kijacho.


Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Mbulu Rehema Bwasi ameeleza kuwa katika jitihada za kupambana na ukatili wa kijinsia Halmashauri imeendelea kuunda madawati kwa ngazi za kata.

“Jamii imeendelea kupewa elimu juu ya kupinga ukatili wa kijinsia kwa watoto kupitia makongamano mbalimbali”. Alisema Bi. Rehema.

Kwa upande wake kiongozi wa Jumuiya ya Makanisa ya Kikristo Mchungaji Augustino Halule ameeleza kuwa elimu juu ya ukatili imeendelea kutolewa kwa Waumini ili kupunguza kasi ya ukatili katika Wilaya ya Mbulu.

Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika yamekuwa na Kaulimbiu isemayo “Haki za mtoto; Tulipotoka, Tulipo na Tuendako.”

Vijana Mbulu wapewa mbinu kukabili changamoto za ajira
Wafanyakazi, Jamii tushirikiane kulinda Miundombinu ya Umeme - TANESCO