Vijana wilayani Mbulu Mkoani Manyara wamehimizwa kuwekeza kwenye shughuli za kiuchumi ili kuondokana na changamoto ya ukosefu wa ajira, kwa kuanzisha miradi au shughuli za uzalishaji mali zenye tija zitakazowawezesha kuchangamkia na kusimamia ipasavyo fursa mbalimbali za kukua kiuchumi na kuchangia pato la taifa.

Wito huo umetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Mbulu, Michael  Semindu, wakati wa kongamano la vijana lenye lengo la kuwawezesha vijana na kuwajengea uwezo  na kupata elimu ya mikopo na uwezeshwaji wa kijasiriamali wilayani humo.

Afisa maendeleo ya  vijana katika halmashauri ya wilaya ya Mbulu Edes Thomas Melly  amesema lengo la kongamano hilo vijana Haydom nyama choma festival  ni kuwawezesha vijana kupata maarifa ya kujitambua, kujiamini na kutumia fursa za maendeleo zilizopo katika jamii zao kwa faida yao binafsi na taifa kwa ujumla.

Baadhi ya vijana walioshiriki kongamano hilo wamesema mafunzo waliyoyapata yamewasaidia kutambua umuhimu wa kutumia fursa zilizopo katika maeneo yao ili kujiletea maendeleo.

Maisha: Mama mkwe afumwa akiloga chumba cha wanandoa
DC Semindu ataka uzingatiaji haki, malezi ya Watoto