Na Swaum Katambo – Katavi.

Mkoa wa Katavi upo mbioni kuondokana na adha ya umeme usio wa uhakika wa jenereta na kuunganishwa kwenye mfumo wa umeme wa gridi ya Taifa ambapo kwa sasa ujenzi wa mradi huo umekamilika kwa asilimia 100.

Mradi huo uliokuwa ukitekelezwa na Kampuni ya ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya usafirishaji na usambazaji umeme (ETDCO) ambayo ni Kampuni tanzu ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) imekamilisha mradi wa umeme wa grid ya Taifa kutoka Tabora hadi Katavi na baada ya muda wa matazamio umeme huo utafikishwa kwa wananchi ili kutatua changamoto za umeme zilizokuwepo.

Akizungumza wakati wa kupima njia ya upokeaji wa umeme katika kituo cha Mpanda Kaimu Meneja Mkuu ETDCO CPA Sadock Mugendi amesema laini hiyo kwa sasa iko tayari kwa ajili ya kuingiza umeme ndani ya Mkoa wa Katavi na kinachoendelea sasa ni matazamio kwa kipindi cha miezi sita.

Kwa upande wao wananchi wa mkoa wa Katavi wamesema kukamilika kwa mradi huo kutaongeza fursa za ajira kutokana na kuongezeka kwa viwanda vitakavyo toa ajira kwa wananchi hao.

Mradi wa njia ya kusafirisha umeme ya msongo wa Kilovoti 132 yenye urefu wa km 383 kutoka Mkoa wa Tabora mpaka Mkoa wa Katavi umetekelezwa kwa gharama ya shilingi Bilioni 116.

Mwenge wa Uhuru wabariki Miradi saba Tanga jiji
Maisha: Mama mkwe afumwa akiloga chumba cha wanandoa