Na Boniface Gideon –  Tanga.

Kiongozi wa mbio za Mwenge,Ismail Ali Ussi , amesema miradi yote 7 iliyokaguliwa katika Wilaya ya Tanga ikiwemo miradi 6 ya Halmashauri ya Jiji la Tanga imekidhi vigezo .

Mwenge wa Uhuru ulizuru jana juni 16 katika Wilaya ya Tanga,na kufanya ukaguzi wa Miradi mbalimbali ya Halmashauri na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira ‘ Tanga Uwasa’.

Miradi hiyo inathamani ya Bilion 3.3, miongoni mwa miradi hiyo iliyofanyiwa ukaguzi ni pamoja na Ujenzi wa jengo la ghorofa la chini vyumba vya madarasa manne, Ujenzi wa Ofisi ya Utawala na matundu ya vyoo katika shule ya Msingi Mbuyuni iliyopo kata ya Nguvumali,
Ujenzi wa Ofisi ya kata ya Tongoni,mradi wa madarasa mawili shule ya Msingi Mwakidila.

Miradi mingine ni pamoja na, mradi wa jengo la mionzi ‘ X-ray’ katika kituo cha Afya Makorora, Ujenzi wa Barabara ya Sahare kwa kiwango cha Lami awamu ya kwanza na ya pili, yenye Urefu wa Mita 600 pamoja na Mradi wa Ufungaji Mita za Malipo ya Kabla za Maji chini ya Mamlaka ya maji na maji Safi Jijini Tanga ‘ Tanga Uwasa’.

Ismail, alisema miradi yote iliyokaguliwa imekidhi vigezo,nakuwata wasimamizi wa Miradi hiyo kuhakikisha inafanya kazi ipasavyo ili kuleta kuhudumia Wananchi,

“Niwaombe wasimamizi wa Miradi hii ,hakikisheni inafanya kazi ipasavyo ili ilete manufaa kwa Wananchi, Wananchi wetu wanataka huduma bora,hivyo ni lazima tufanye kazi ambayo Rais ametutuma , lakini hakikisheni mnawahamasisha Wananchi kushiriki Uchaguzi Mkuu utakaofanyika baadae mwaka huu” Aliongeza Ismail

Kwaupande wake Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Dkt.Batilda Buriani alisema Mkoa wa Tanga huo una fursa nyingi za kiuchumi ambapo aliwaomba wakazi wa Mkoa huo,kuchangamkia fursa hizo ikiwemo Kilimo,

“Mkoa wetu ,una fursa nyingi za kiuchumi,hivyo niwaombe Wakazi wa Mkoa wa Tanga,mchangamkie fursa ,tuna Kilimo cha mazao ya chakula na Biashara, ikiwemo Mkonge,Korosho,Mihogo , mahindi na matunda ya aina mbalimbali yanapatikana katika Mkoa wetu,” alisema Dkt. Batilda.

kuhusu Uchaguzi Mkuu, Dkt. Buriani aliwataka Vijana kujitokeza kwa wingi kuwania nafasi mbalimbali kupitia vyama vyao vya kisiasa,

“Niwaombe Wananchi hasa Vijana,mjitokeze kwa wingi kushiriki Uchaguzi Mkuu,muwanie nafasi mbalimbali kupitia vyama vyenu vya kisiasa,” aliongeza Dkt. Buriani.

Wazazi toeni taarifa za wanaofanya vitendo vya ukatili - DC Kilakala
Hatimaye Katavi kuondokana na kero ya Umeme