Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Musa Kilakala amewataka wakazi wa wilaya hiyo kutoa taarifa za watu wanaofanya vitendo vya ukatili, ili kuwezesha mapambano dhidi ya vitendo hivyo.
Akizungumza katika Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika ndani ya Manispaa ya Morogoro, Kilakala amesema ili kukabiliana na mmonyoko wa maadili ni lazima kukemea vikali hali ya ukiukwaji wa maadili mema hasa katika kuzingatia mila, tamaduni na desturi.
Naye Afisa wa Maendelea ya jamii, Mratibu wa Dawati la Maendeleo ya Mtoto Manispaa ya Morogoro, Joyce Levocatus mgambe ameelezea namna Hali ilivyo Kwa Manispaa ya Morogoro.
Ikumbukwe Kila Mwaka tarehe 16 mwezi juni ni Maadhimisho ya Mtoto wa Afrika Na kauli mbiu ya mwaka huu ikiwa ni Haki ya Mtoto: “Tulipotoka, Tulipo na Tuendako”.