Afarah Suleiman, Babati – Manyara.
Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Mji wa Babati Mkoani Manyara limevunjwa rasmi huku wakiwataka watendaji kutatua kero za wananchi zilizowezesha Halmashauri hiyo kupata Hati safi.
Madiwani hao wamewataka Watendaji na Wataalam kwa ujumla kutatua kero za wananchi na kusimamia miradi ya maendeleo vizuri zilizowezesha Halmashauri hiyo kupata hati safi.
Agizo hilo limetolewa kwenye hitimisho la Baraza la nne la madiwani lililoanza 2020 hadi kufikia leo juni 19, 2025.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Babati CPA.Shaaban Mpendu amesema kuwa katika kipindi cha miaka mitano baraza hilo limepata mafanikio tofauti na mabaraza mengine.
Akivunja Baraza hilo Katibu Tawala wa Wilaya Babati Khalfan Matipula kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Babati Emmanuela Kaganda amewataka Madiwani wote kuwa kioo cha jamii lakini pia watendaji kuhakikisha wanasimamia miradi ya maendeleo na kuhamasisha wananchi kujitokeza kushiriki Uchaguzi Mkuu pamoja na kutoa elimu.
Sambamba na hilo ametoa vyeti vya pongezi kwa utumishi mzuri kwa madiwani 11 wa Kata zote nane za Halmashauri ya Mji Babati.