Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Dkt. Benedicto Ngaiza, amewataka wataalamu wa sekta ya afya ea mikoani ya Mtwara, Lindi na Wilaya ya Tunduru kusimamia vyema ukusanyaji wa mapato kwenye vituo vya kutolea huduma za afya, ili kulipa Madeni ya Bohari ya Dawa (MSD) na kuipa msuli wa kiuchumi katika kutekeleza majukumu yake katika mnyororo wa ugavi wa bidhaa za afya kwa weledi, ufanisi na kwa wakati.

Dkt. Ngaiza, amesema kutolipa madeni ya MSD kwa wakati, kunadhoofisha juhudi zinazofanywa na MSD na serikali kwa ujumla kuboresha huduma za afya nchini, mathalani upatikanaji wa bidhaa za afya.

Dkt.Ngaiza ametoa rai hiyo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara wakati wa ufunguzi wa kikao cha wateja na wadau wa MSD Kanda ya Mtwara kwa mwaka 2025, kilichofanyika Mkoani Mtwara.

Akizungumza kuhusu maoteo ya bidhaa za afya, Dkt.Ngaiza amewataka wasimamizi hao wa sekta ya fya, kusimamia maoteo ya bidhaa za afya kwa usahihi na kwa wakati ili kuiwezesha MSD kununua bidhaa hizo kwa usahihi na kuzisambaza kwa wakati, lakini pia kuepusha kuchina kwa bidhaa.

Awali akitoa taarifa ya utendaji wa MSD Kanda ya Mtwara, Meneja wa Kanda hiyo Bi. Thea Malay amesema uwepo wa madeni makubwa kwa baadhi ya wateja, umeathiri kwa kiasi kikubwa utekelezaji wa majukumu ya kanda hiyo, hivyo kuwataka wadau hao kufanya msawazo wa madeni hayo,

Hata hivyo, Bi.Malay amewashukuru wadau na wateja hao kwa kuendelea kushirikiana na MSD, huku akiahidi Kanda hiyo kuendelea kuimarisha mawasiliano na mahusiano baina ya pande hizo, ili kwa pomoja waweze kuboresha huduma za afya.

Chifu Mkuu Hangaya ashiriki Tamasha la Utamaduni Bulabo
TBL, TARI waadhimisha siku ya Wakulima wa Mtama Hombolo Dodoma