Biashara ya bidhaa bandia imeendelea kusababisha athari hasi katika uwekezaji hususani katika mataifa mengi duniani kwakuwa imekuwa ikishindanisha bidhaa bandia na zile zinazozalishwa kihalali.
Akizungumza na Waandishi wa habari Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani (FCC) na Mkaguzi Mkuu wa Sheria ya Alama za Bidhaa, Khadija Ngasongwa kuhusu kuelekea Maadhimisho ya Kitaifa Ya Siku ya Udhibuti wa Bidhaa Bandai Dunia ambapo inafanyika Juni 20, 2025 ambapo amesema, kutokana na uwekezaji mkubwa unaofanywa na wazalishaji wa bidhaa halisi.
Pia, gharama kubwa za uendeshaji huzifanya kampuni zinazozalisha bidhaa halisi kushindwa kushindana na bidhaa bandia ambazo huharibu sifa ya zile halisi na kuwaondosha wawekezaji wake sokoni na kusababisha upotevu wa mapato tarajiwa kwa njia ya kodi, ajira na hupunguza wigo wa bidhaa katika soko kwa walaji.
Hata hivyo, amesema FCC inashirikiana na Jumuiya mbalimbali za wafanyabiashara pamoja na wataalam wa Ushuru wa Forodha (TAFFA) katika kutoa na kufikisha elimu kwa Umma na wadau wao kuhusu sheria na athari mbalimbali wanazopaswa kuzizingatia katika shughuli zao ili waepuke kuwa wahanga wa uingizaji wa bidhaa bandia nchini unaoweza kuwasababishia hasara kubwa endapo wakikamatwa.
Amesema Maadhimisho ya mwaka huu ya Kitaifa ya Siku ya Udhibiti wa Bidhaa Bandia Kimataifa imebeba Kaulimbiu isemayo “Kujenga Kesho Salama, Kutetea Uhalisia kwa Uongozi Thabiti”.
“Maadhimisho haya yatafanyika Jijini Dodoma ambapo tarehe 19 Juni 2025 tumeanza kwa kutoa elimu kwa Umma kupitia redio mbalimbali hapa Dodoma, na tutaendelea kufanya hivyo hadi Juni 25 tutakapofikia tamati ambapo kutafanyika Kongamano la wadau mbalimbali wakiwemo wadau wa maendeleo kutoka katika mashirika na asasi mbalimbli za kimataifa”, amesema.
“Wamiliki au wawakilishi wa Miliki Bunifu mbalimbali nchini (Itellectual Property Holders and Brand Owners), wanasheria, wafanyabiashara, wazalishaji na vyama mbalimbali vya uwakilishi vya wazalishaji na wafanyabiashara wa makundi mbalimbali pamoja na Taasisi za Serikali zinazounda Kikosi Kazi cha Kitaifa cha Udhibiti wa Bidhaa Bandia kinachoundwa kwa mujibu wa Sheria ya Alama za Bidhaa”. Amesema Ngasongwa.