Afarah suleiman, Babati – Manyara.

Jumla ya vijiji 10 vinavyounda Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori Burunge (Burunge WMA) wilayani Babati, mkoani Manyara, vinatarajiwa kunufaika na mradi wa ufugaji wa kuku wa kisasa kwa lengo la kuinua kipato cha wananchi na kukidhi mahitaji ya soko la nyama ya kuku katika hoteli za kitalii zilizo jirani.

Akizungumza katika kikao kazi, Mkuu wa Wilaya ya Babati, Mhe. Emmanuela Kaganda, amesema mradi huo ni sehemu ya jitihada za kuwainua wananchi kiuchumi kupitia sekta ya utalii. Amewataka wadau wa utalii kushirikiana na jamii kwa kununua bidhaa zinazozalishwa na wananchi ikiwemo kuku.

Kampuni ya Silverland, inayojishughulisha na usambazaji wa vifaranga na chakula cha kuku, imeahidi kushirikiana na wananchi kwa kutoa mafunzo ya ufugaji bora, kutoa vifaranga 500 na chakula kwa wananchi 60 kutoka vijiji hivyo.

Kwa upande wao, wadau wa utalii kutoka Chem Chem Association wameahidi kutoa soko la uhakika kwa kuku hao, ili kuwezesha wananchi kunufaika moja kwa moja na sekta ya utalii kupitia kilimo na ufugaji.

Maisha: Jinsi alivyomthibiti mkewe aliyekuwa akimpiga, kuninyima tendo
TRA: Asilimia 70 ya Bajeti kuu ya Serikali inatokana na makusanyo ya Kodi