Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema maboresho ya Bandari za Tanzania na ushirikishwaji wa sekta binafsi kwenye uendeshaji wa gati umepunguza muda wa meli kupunguza kutoka 46 hadi saba.
Kwa upande wa muda wa meli za makasha kusubiri, Rais Samia amesema umepungua kutoka siku tano na sasa kuingia moja kwa moja gatini pindi zinapowasili katika Bandari ya Dar es Salaam.
“Makasha yanayohudumiwa yameongezeka kwa asilimia 35 kutoka 159,807 hadi 215,286 na jumla ya uzito wa shehena iliyohudumiwa imeongezeka kwa asilimia 14 kutoka tani milioni 14.42 hadi milioni 16.87,” amesema.
Kutokana na uwekezaji huo, Rais Samia amesema umewezesha kuongezeka kwa makusanyo ya kodi kutoka Sh850 bilioni mwaka 2023/24 hadi Sh1 trilioni kwa mwezi mwaka 2025.
Alisema, “matumizi kwa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA), amesema yamepungua kwa mwezi kutoka Sh262.15 bilioni hadi Sh166.3 Mei 2024 hadi Machi 2025. Rais Samia ameyasema hay oleo Ijumaa, Juni 27, 2025 wakati akilihitubia Bunge jijini ikiwa ni sehemu ya mchakato wa kuhitimisha shughuli za Bunge la 12.”