Zaidi ya Wanachama 65 wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Wilaya ya Missenyi wamehamia chama Cha Mapinduzi CCM huku wakisema wanaunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kutokana na juhudi kubwa za Maendeleo ndani ya Wilaya hiyo.
Akiwapokea wanachama hao juni 29,2025 Katibu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Missenyi Bakari Mwacha amekili kuwapokea wanachama 22 Kutoka sehemu mbalimbali katika Jimbo la Missenyi na kwamba watasajiliwa kwa mfumo wa elektronik kwa utaratibu wa Chama Cha Mapinduzi.
Kwa upande wao baadhi ya Wanachama hao akiwemo Remigius Daniel Kamzola aliyekuwa Katibu wa Chadema kata ya mabale na Apolinary Joseph Kaijage pia Halima John ambao walikuwa wanachama wa Demokrasia na Maendeleo CHADEMA wameeleza sababu yao ambayo imepelekea wao kuhama Chama hicho na kuingia CCM kwamba ni Maendeleo ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania lakini pia kijana mpambanaji, mchumi na mkulima Evance Kamenge kuchukua fomu ya kugombea ubunge katika Jimbo jambo ambalo wanaimani kuwa ataleta mabadiliko makubwa.
Ikumbukwe kuwa Jana juni 28,2025 dirisha la kuchukua fomu za kugombea limefunguliwa rasmi ambapo Mchumi na mkulima Evance Kamenge kijana mpambanaji tayari amechukua fomu ya kutia nia ya kugombea ubunge katika Jimbo la Missenyi.