Mbunge wa Jimbo la Missenyi Mkoani Kagera Florent Kyombo leo juni 30 amechukua fomu ya kutetea kiti chake cha ubunge katika Ofisi za chama cha Mapinduzi CCM Wilaya humo.

Ilikuwa ni majira ya saa sita za mchana katika Ofisi za chama hicho Dar 24 Media imefika na kuweka kambi kwa muda ya kujionea mchakato mzima wa zoezi la uchukuaji na urejeshaji wa fomu za uchaguzi kwa baadhi ya wagombea waliojitokeza kuwania nyazifa mbalimbali za udiwani ubunge pamoja na viti maalumu ili kulitetea jimbo na kata.

Frolent Kyombo ambaye ni mbunge wa jimbo hilo kwa muda wa miaka mitano na ukomo wa ubunge wake ni Agost 03 mwaka 2025 kama ilivyo tangazwa na Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan wakati akihitimisha shuguli za Bunge la 12 ambapo mbunge huyo amesema amechukua fomu ili kutete nafasi yake na chama Kimpatie ridhaa kwa mara nyingine na kuwatumikia wananchi.

Kyombo amesema amerejea kutetea kiti hicho akiona kwenye jimbo hilo Serikali imetekeleza na kuleta maendeleo makubwa katika sekta ya Afya elimu maji pamoja na miundombinu mbalimbali ya barabara ajira na umeme kwenye vijiji mpaka kuvifikia vitongoji.

“Kwanza nawashukuru sana wananchi kwa umoja amani na mshikamano walionipatia ili niweze kutekeleza majukumu yangu na leo hii ninaporudi kwao nikiomba waniongezee muda wa kuendelea kuwaletea mambo mengine mazuri ambayo nimeyaacha njiani yatakayotekelezwa kwenye mwaka mpya wa bajeti unaokuja”amesema Kyombo.

Hata hivyo Kyombo amesema katika miradi ambayo inaendelea kutekelezwa ni barabara ya lami kutoka But Butwale mpaka Katoma na Bunazi junction hadi Kagera Suger mkandarasi emeshalipwa kazi ya kwanza bilioni 5.4 barabara nikaribia kuanza na kwenye bajeti itajengwa barabara ya kiusalama kilometa 56 kutoka Mutukula hadi Kakunyu.

Dkt. Ndumbaro achukua fomu ya Ubunge Songea Mjini
Ummy Mwalimu achukua fomu kutetea nafasi yake jimbo la Tanga