Na Swaum Katambo – Katavi.

Maafisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Katavi,wameungana na wafanyabiashara waliopo mkoani humo kusherehekea mafanikio ya makusanyo ya mapato yaliyotangazwa na Kamishna Mkuu wa mamlaka hiyo Yusuph Mwenda jijini Dar esSalaam.

Wakifuatilia mubashara uwasilishwaji wa taarifa ya makusanyo ya mapato kwa mwaka wa fedha 2024/25 ambapo Kamishna Mkuu wa mamlaka hiyo Yusuph Mwenda amesema tangu mamlaka hiyo ianzishwe haijawahi kuvunja rekodi ya kukusanya mapato kama ilivyo kwa mwaka wa fedha uliopita ambapo imekusanya zaidi ya shilingi trilioni 32.2, kiwango ambacho hakijawahi kukusanywa.

Kamishna Mwenda amesema kuwa, TRA inapoanza mwaka mpya wa fedha itaendelea kutatua changamoto za wafanyabiashara pamoja na kuweka usawa wa ulipaji kodi jambo linaloungwa mkono na wafanyabiashara waliopo mkoani Katavi pamoja na maafisa wa TRA mkoa humo.

Kwa upande wake Meneja msaidizi wa TRA Mkoa wa Katavi Joshua Mille amesema wataongeza ufanisi katika ukusanyaji wa mapato kama ilivyoelekezwa ili kuhakikisha malengo yaliyokusudiwa yanatimia pamoja elimu kufika kwa wafanyabiashara na kutatua changamoto zao.

Siasa: Mfahamu Ugin Mkinga Mtia nia Ubunge Jimbo la Madaba
George Bajuta ataka uwakilishi Jimbo la Hanang'