Jumla ya Shilingi Bilioni 196.4 zimetumika kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya Umeme ikiwemo Upanuzi wa mtandao wa Umeme kwa Wilaya ya Mpanda, Tanganyika na Mlele.

Akizungumza leo na Waandishi wa habari Jijini Dodoma, Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Mwanamvua Mrindoko, ambapo amesema pamoja na Kuongeza nguvu ya Umeme kwa Wilaya ya Mpanda, Tanganyika na Mlele, kupeleka Umeme kwenye Vijiji kwa ufadhili wa REA awamu ya kwanza katika Vijiji vyote 172 vya Mkoa na vina Umeme.

“Hadi kufikia Juni, 2025 Vitongoji 504 kati ya Vitongoji 912 vya Mkoa wa katavi vimeunganishiwa umeme na Vitongoji 408 vilivyo baki vitaunganishwa katika bajeti ya mwaka wa fedha wa 2025/2026,” amesema.

“Upelekaji wa huduma hizi umeongeza idadi ya wateja wanao tumia Umeme kutoka wateja 23,312 mwaka 2020/21 hadi wateja 42,567 Juni, 2025 na kumeleta chachu ya ongezeko la mapato kutoka shilingi 494,496,385.22 hadi shilingi 1,031,280,772.87 kwa mwezi.” Amesema Mrindoko.

Hata hivyo amesema kumeleta ongezeka la uchakataji wa mazao ya kilimo ambapo Idadi ya viwanda katika Mkoa wa Katavi imeongezeka kutoka 873 mwaka 2021 hadi 1,782 mwezi Juni, 2025.

Amesema Katika mwaka wa fedha TANESCO Mkoa wa Katavi uliidhinishiwa kutumia kiasi cha shilingi 10,838,286,911.00 kwa ajili ya miradi ya kuboresha huduma ya Umeme kwa mchanganuo ufuatao.

Hata hivyo amesema Wakala wa Barabara (TANROADS) Mkoa unahudumia mtandao wa barabara wenye jumla ya kilometa 1,201.81. Kati ya hizo kilomita 594.46 ni barabara kuu na kilomita 607.35 ni barabara za mikoa.

Wananchi wa Mkoa wa Katavi wanashukuru kwa kuwajenga barabara ya Mpanda – Tabora yenye Kilometa 352 ambayo imekuwa ni chachu kubwa ya ukuaji wa uchumi wa wananchi kupitia sekta ya usafiri na usafirishaji na kuufungua Mkoa wa Katavi kwa fursa mbalimbali.

“Mkoa wa Katavi unapongeza juhudi za Serikali chini ya uongozi wa Rais wa awamu ya Sita kwa kuleta kiasi cha shilingi billioni 410,975,698,026.00 kwa ajili ya miradi ya kimkakati na ya kitaifa”,

“Miradi hii itakapokamilika mtandao wa barabara kwa kiwango cha lami utaongezeka kutoka kilomita 325.81 na kufikia kilomita 548.45”. Amesema

Katika mwaka wa fedha 2023/24 Mkoa wa Katavi ulitekeleza miradi 39 yenye jumla ya Shilingi bilioni 15.092 kwa ajili ya kufanya matengenezo ya Barabara kuu na za Mkoa zenye jumla ya kilomita 1,201.81 pamoja na Kufanya matengenezo ya kinga katika madaraja na kujenga madaraja mapya.

Utekelezaji wa Miradi kwa ufanisi: NIC ni mfano wa kuigwa - Prof. Kabudi
Aomba mkopo Halmashauri kupunguza ombaomba