Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wafugaji Tanzania (CCWT), Ally Manonga, amesema uamuzi wake wa kuwania ubunge wa Jimbo la Hanang’ kupitia chama tawala umetokana na nia ya dhati ya kuleta mageuzi ya kiuchumi na kijamii kwa wananchi wa jimbo hilo na Watanzania kwa ujumla.
Akizungumza baada ya kuchukua na kurejesha fomu ya kuomba kuteuliwa kuwa mgombea, Manonga ameeleza kuwa uzoefu wake katika kutetea haki za wafugaji umemuwezesha kuelewa kwa undani changamoto zinazowakabili wakulima, wafugaji na vijana, hivyo kuwa na kiu ya kuzipatia majibu kupitia nafasi ya ubunge.