Mkoa wa Singida umeendelea na usimikaji wa mifumo mbalimbali na matumizi
ya TEHEMA kama njia ya kufikia maendeleo ya haraka kwa Kuendelea kuanzisha matumizi ya kompyuta katika maeneo ya kutolea huduma (Elimu, Kilimo, Mapato, Maofisini.
Akizungumza leo Juli 4,2025 na Waandishi wa habari Jijini Dodoma Mkuu wa Mkoa wa Singida, Halima Dendego ambapo pia amesema Mkoa huo unaendelea Kusimika mifumo mbalimbali ya kielektroniki.
“Mfumo wa ukusanyaji mapato TAUSI umekamilika, Mfumo wa upokeaji malalamiko (e-mrejesho) umekamilika, Mfumo wa uendeshaji vituo vya kutolea huduma za Afya
GoTHOMIS unaendelea kusimikwa”, amesema
“Mfumo wa minada ya mazao TMS unatumika
Na mingineyo mingi kama MUSE, HCMIS. NeST, FFARS, inatumika, Minara 55 ya simu inaendelea kujengwa, Kituo cha kuongeza usikivu wa Radio ya Taifa kimekamlilika”. Amesema Dendego
Vilevile amesema Mkoa wa Singida umeendelea kuwa na mafanikio makubwa katika sekta ya miundombinu kwa upande wa TARURA katika maeneo mbalimbali.
“Kuongeza barabara za lami toka km29.8 hadi km 51.1, Kuongeza barabara za changarawe toka km 700 hadi km 1,892.28, Ujenzi wa madaraja mapya 17 na makalavati 2,336, Kufungua barabara mpya zenye urefu wa km 609.16”, amesema
“Aidha TANROADS imeendelea na ujenzi wa barabara kuu na zile za mkoa
kwa kuendeleza ujenzi wa barabara zenyewe, madaraja na vivuko, kwa uchache maeneo yafuatayo yameendelea kuimarishwa, Kujenga kivuko cha chini cha watembea kwa miguu katika barabara ya Dodoma – Mwanza eneo la Kibaoni halmashauri ya Manispaa ya Singida
Kujenga daraja la Msingi lililopo halmashauri ya Mkalama lenye urefu wa mita 100 na kilomita 1 ya lami”. Amesema
Pia amesema “Utekelezaji wa ujenzi wa barabara kiwango cha lami KM 10
Nduguti mjini, Utekelezaji wa ujenzi wa barabara kiwango cha lami KM 10
Igauri – Ilongero, Ukamilishaji wa maandalizi ya ujenzi wa daraja za Sanza”