Moja kati ya Mashirika yanayostahili kupewa miradi mbalimbali ya kitaifa ni pamoja na Shirika la Bima Taifa (NIC) kutokana na kuonesha uwezo mkubwa pindi wakati wa utekelezaji wa miradi mbalimbali.

Hayo yamebainishwa jijini Dar es Salaama na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Prof. Palamagamba Kabudi  wakati alipotembelea Banda la Shirika hilo, kwenye maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba na kuongeza kuwa NIC wanastahili kutokana na uwezo walionao.

 

Kabuki poa , amelipongeza Shirika hilo kwa kuunga mkono sekta ya michezo kutokana na udhamini wao kwa Klabu zote zinazoshiriki Mapinduzi Cup.

Awali, Mkurugenzi wa Masoko na Mawasiliano wa NIC, Karim Meshack aliesema NIC inaunga mkono juhudi za Serikali katika kukuza sekta ya michezo nchini.

Maisha: Simulizi ya mbinu rahisi ya kuinua biashara
Bilioni 196.4 zatumika kutekeleza miradi mbalimbali Wilaya za Katavi