Katika ripoti mpya ya Global Peace Index (GPI) 2025, Tanzania imetajwa kuwa nchi yenye amani zaidi Afrika Mashariki, ikishika nafasi ya 73 kati ya nchi 163 duniani.

Ingawa Tanzania imeporomoka kwa nafasi 8 ikilinganishwa na mwaka uliopita, bado inaongoza kanda hii, huku majirani wengine wakipanda au kushuka katika viwango vya amani.

🔹 Viwango vya Amani Afrika Mashariki (2025):

1. 🇹🇿 Tanzania (73)
2. 🇷🇼 Rwanda (91)
3. 🇺🇬 Uganda (113)
4. 🇰🇪 Kenya (127)
5. 🇧🇮 Burundi (133)
6. 🇨🇩 DRC (160)
7. 🇸🇸 Sudan Kusini (161)

Ripoti hii inayotolewa kila mwaka na Institute for Economics and Peace (IEP) hutathmini amani kwa kutumia vigezo 23, vikiwemo usalama wa kijamii, kiwango cha migogoro, na hali ya kijeshi.

Licha ya changamoto mpya zinazojitokeza, Tanzania inaendelea kuwa mfano wa amani na utulivu wa kisiasa katika ukanda huu. Hata hivyo, wataalamu wanashauri kuimarishwa kwa taasisi za kitaifa ili kukabiliana na mabadiliko ya mazingira ya usalama kikanda.

🌍 GPI 2025 pia imebaini kuwa amani duniani imeshuka kwa mara ya 13 ndani ya miaka 17, kutokana na migogoro ya ndani na shinikizo za kijiofisia.

Nishati Safi ya kupikia ni ajenda ya Dunia - Dkt. Kazungu
Mazingira wezeshi ya Serikali yafungua fursa mpya za uwekezaji kupitia TAWA