Mitihani ya Bodi ya Ununuzi na Ugavi Nchini (PSPTB), inatarajiwa kufanyika Agosti 25 hadi 29 mwaka huu ikiwa ni ya 31, huku ikielezwa kuwa kituo kimoja pekee kilichopo Dodoma ndicho kitatumika kama inavyoonesha kwenye dirisha la usajili ambapo mwisho wa maombi ni Agoti 15, 2025.

PSPTB imeeleza kuwa waombaji wenye sifa na nia ya kufanya mitihani hiyo wafanye usajili kupitia https://registration.psptb.go.tz huku wakitakiwa kuhudhuria madarasa ya mafunzo kama sehemu ya maandalizi ya mitihani hiyo

Akiongea na vyombo vya habari jijini Dar Es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji  wa PSPTB, Godfrey Mbanyi amewataja waombaji wenye sifa za kufanya mitihani hiyo Agosti 2025 kuwa ni pamoja na wahitimu wote waliomaliza vyuo vya elimu ya juu na kati kwa ngazi ya Shahada, Stashahada na Astashahada ya ununuzi na ugavi.

“Na hao ni wale wa kipindi cha kuanzia 2024 kurudi nyuma ambao hawakuwahi kufanya mitihani ya kitaaluma ya Bodi ya wataalamu wa Ununuzi na Ugavi. Wengine ni wafanyakazi wanaofanya kazi za Ununuzi na Ugavi katika sekta binafsi na Umma pasipokua na cheti cha CPSP,” amesema.

Aidha, Mbayi amesema pia wapo wahitimu wenye taaluma nyingine ya nje ya ununuzi na ugavi kwa ngazi za stashahada, shahada na Astashahada au wale wenye sifa za kitaaluma kutoka Bodi/ Mabaraza ya taaluma husika na yanayotambulika na PSPTB.

“Watahiniwa wengine wa PSPTB waliomaliza mitihani ya kitaaluma ya Awali ngazi ya pili, ngazi ya msingi (1&2), ngazi ya kwanza , pili, tatu na ya nne ( Professional stage 1,2, 3 na 4) ndani ya miaka mitano kwa mujibu wa matakwa ya mtaala kitaaluma,” aliongeza Mbanyi.

Aidha, amewataja pia watahiniwa wote wanaorudia baadhi ya masomo katika ngazi mbalimbali ndani ya miaka mitatu kwa mujibu wa matakwa ya mtaala mpya, huku akiwataja wale wanaorudia mitihani zaidi ya ngazi moja kuwa wanaruhisiwa kuunganisha ngazi mbili zinazofiatana ( Two Consecutive Blocs) kwa masomo kuanzia mawili hadi sita.

Kuhusu ada za mitihani, Mbayi amesema zimewekwa kwenye tovuto ya Psptb na uendeshaji wa mitihani mingine inafanyika Novemba na Mei itaendelea kama kawaida, na endapo kutakua na changamoto katika kufuata mchakato huo wasiliana na watendaji Pspst kwa nambari 0738 441972.

Watumishi wa BRELA wasisitiziwa nidhamu kazini
Kesi ya kupinga kanuni za maadili ya uchaguzi yaanza