Chuo Cha Ufundi Stadi (VETA), Mkoani Mtwara kupitia Wanafunzi wake wamtengeza Kiti kinachobadilika kulingana na mahitaji ambacho kinaweza kuwa Sofa, Kiti na Meza kwa nyakati tofauti.
Mhandisi kutoka chuo VETA, Elias Boniface amyasema hayo wakati akizungumza na Waandishi wa habari kwenye maonyesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara Sabasaba,  jijoni Dar es Salaam.
Amesema, “VETA Mtwara tuna bidhaa ambazo tumezileta ambazo ni bunifu zimetokana na kazi ambazo wanafunzi wenyewe wamezifanya,moja ya bunifu ambayo tumekuja nayo ni kiti ambacho kinabadilika kuwa sofa,kiti pamoja na Meza.”
Boniface  ameongeza kuwa, ubunifu huo umerahisisha maisha, kwani wengi wanapoanza maisha huwa na vyumba vidogo hivyo sofa hilo litawasaidia kuwa na vitu vitatu kwa wakati mmoja.
“Pia VETA Mtwara imekuja na bunifu nyingine ambayo ni mashine kwa ajili ya kukata chupa, mashine hiyo imewasaidia baadhi ya watu wengi, kwasababu ni mashine inayotatua moja kwa moja matatizo yaliyopo kwenye jamii,” alieleza Mhandisi Boniface.
“Tunaikata chupa iliyotumika na kuirudisha sokoni kama glasi. Mashine hiyo inatumia umeme kukata hizo chupa, ambapo kunakuwa na glascuter, kunakua na handle pamoja na sehemu ambayo ni kufunga na kuifungua,” alifafanua Boniface.

Mkurugenzi Marwa afanya ziara banda la TTCL Sabasaba 
Maisha: Je, unasumbuka kupata ajira?, tumia njia hii upate ushindi