Thierry Henry amemkingia kifua kocha wake wa zamani Arsene Wenger, na kusisitiza kuwa Arsenal wana kikosi ambacho kina uwezo wa kushinda taji la ligi kuu nchini Uingereza punde tu baada ya dirisha la usajili kufungwa rasmi jana.
‘The Gunners’,  wameshindwa kufanya usajili wa maana kuongezea nguvu katika kikosi chao katika dirisha hili la usajili, isipokuwa mlinda mlango Petr Cech pekee ndio wamefanikiwa kuinasa saini yake.
Arsenal ndio klabu pekee kati ya klabu kubwa za Ulaya ambayo imeshindwa kufanya usajili wa nguvu, lakini Henry amekuwa na shaka juu ya utayari wa ama mshambuliaji wa Madrid Karim Benzema au Edinson Cavani wa kama kweli walikuwa na nia ya kujiunga na miamba hiyo ya London ya Kaskazini wenye wanaokipiga katika dimba la Emirates.
“Sina uhakika kama kweli Wenger alikuwa anamtaka Benzema au vinginevyo, lakini hiyo pia inatokana na utayari wa mchezaji kuja,” alisema wakati akifanya uchambuzi katika kituo cha Televisheni cha Sky Sports.
“Ni kipi hasa ambacho unaweza kumpa mchezaji ambaye anacheza katika moja ya vilabu vikubwa ulimwenguni, wakati huo akifahamu fika kwamba ana uhakika wa kucheza kila wiki tena katika kikosi cha kwanza?.
Haendi popote: Benzema alikuwa akihusishwa na kujiunga na Arsenal, lakini ameamua kubaki Real Madrid.
“Hivyo sidhani kama Arsene hakutaka kuleta mchezaji mpya – ingekuwa kama amesema hatosajili mchezaji yeyote basi hapo sawa.’ lakini alisema kuwa kama inawezekana basi nitajaribu kuleta mchezaji mpya.
“Lakini ni jinsi gani unaweza kumsajili Benzema kutoka Real Madrid wakati huo huo ana nafasi kubwa ya kucheza pale, vivyo hivyo kwa Cavani kutoka Paris Saint-Germain – ni wikiendi iliyopita tu hapo alifunga goli, ni vigumu sana.
“Mi sidhani kama alikuwa hana mpango wa kuongeza yeyote yule, alitaka kusajili lakini kama wengi tunavyofahamu ilishindikana.

Cech: Mlinda mlango ambaye ndio mchezaji pekee ambaye Arsenal wameweza kumsajili.
“Kwa sasa wana pointi tano nyuma ya City, bado hawajashinda hata mchezo mmoja wa nyumbani, wameshinda michezo miwili yote magoli yakiwa ni ya kujifunga, ambayo kwa sasa ndio tunaweza kusema ndio magoli yao bora.
“Kimtazamo haionekani kuwa sawa kama kweli watachukua ubingwa kwa mtindo huu. Lakini nadhani kwamba Arsene  bado anaamini anaweza kuchukua ubingwa kwa mtindo huu, lakini timu ni nzuri. Ila huo ni mtazamo wake.
“Nadhani angejaribu kuleta japo wachezaji wachache tu na nadhani alijaribu kufanya hivyo, lakini haikutokea hivyo, kwa mtazamo wangu timu bado ilikuwa inahitaji wachezaji kadhaa”.

Simba Yaanika Kikosi Cha 2015-16
Kozi Ya Leseni B Zanzibar Yafutwa