Kocha msaidizi wa timu za taifa za vijana Oscar Milambo ametangaza kikosi cha vijana chini ya umri wa miaka 23, ambacho kitaingia kambini mwishoni mwa juma hili, tayari kwa maandalizi ya awali ya michezo ya kufuzu michuano ya Olimpiki ya mwaka 2020 itakayofanyika Jijini Tokyo nchini Japan.

Milambo ametangaza kikosi cha wachezaji 35, huku akiwajumuisha wachezaji wa klabu nguli za Simba na Young Africans Geoffrey Mwashiuya, Emmanuel Martin na Yusufu Mlipili.

Milambo aliyefanya shughuli hiyo kwa niaba ya mkuu wake, Mdenmark, Kim Poulsen amesema kwamba kikosi hicho kitaingia kambini Novemba 6, mwaka huu katika hosteli za TFF zilizopo Uwanja wa Karume na kitapunguzwa na kubakiwa na wachezji 25. Milambo amesema wachezaji wote walioteuliwa wana umri usiozidi miaka 20, kwa sababu wameteua vijana ambao hata timu ikifuzu Olimpiki ya Tokyo 2020 wataweza kucheza michuano hiyo kwa kuwa ndiyo watakuwa wamefikisha miaka 23 ambayo ndio kikomo.

Kikosi kamili cha U-23 kinaundwa na makipa; Metacha Mnata (Azam FC), Joseph Ilunda (JKT Ruvu) na Liza Mafwea (Tanzania Prisons).

Mabeki ni Paulo Lyungu (Maji Maji), Yussuf Mlipili (Simba), Abbas Kapombe (Ndanda mkopo kutoka Azam), Salum Chukwu (Singida United), Cleotas Sospeter (Yanga), Idrissa Mohammed (Maji Maji), Bakari Kijuji (Tanzania Prisons), Joseph Prosper (Azam FC), Masoud Abdallah ‘Cabaye’ (Azam FC), William John (Ruvu Shooting) na Yusuph Anthony (Yanga).

Viungo ni Adam Salamba (Stand United), Omary Mponda (Ndanda FC), Eliud Ambokile (Mbeya City), Geoffrey Mwashiuya (Yanga), Emmanuel Kakuti (Mbeya City), Emmanuel Martin (Yanga), Medson Mwakatunde (Mbeya City) na Derueshi Shaliboko.

Washambuliaji ni Ismail Aidan (Mtibwa Sugar), Salum Kihimbwi (Mtibwa Sugar), Hassan Mganga ((Mtibwa Sugar), Awad Salum (Njombe Mji FC), Awesu Ally (Mwadui FC), Yahya Zayed (Azam FC),Ayoub Masoud (Ndanda FC), Baraka Majogoro (Ndanda FC), Mohammed Habib (Miembeni FC), Agathon Mapunda (Njombe Mji), Faisal Salum Abdallah (JKU) na Yusuph Kagoma (Singida United).

Mpina awataka wafugaji kutembea kifua mbele
Simba SC waifuata Mbeya City kwa usafiri wa anga