Jumla ya Matapeli 11 wanaojihusisha na kutuma ujumbe wa Simu maarufu kama “PESA HIYO TUMA KWENYE NAMBA HII JINA….’ wamekamatwa na Polisi Mkoani Tanga wakiwa na laini za Simu zaidi ya 400 na Vifaa mbalimbali vya mawasiliano.

Kwa mujibu wa kamanda wa Polisi Mkoani Tanga, Henry Mwaibambe amesema matapeli hao wametoka katika mikoa Dar es Salaam na Tanga na kuweka Kambi kwenye moja ya Nyumba ya kupanga, iliyopo kata ya Mnyanjani eneo la Donge.

Katika orodha hiyo ya Matapeli wamo wanawake wawili na tisa Wanaume ambapo wametambuliwa kwa majina ya Hadija Nyange (34), mkazi wa muheza, Zaina Athuman (25), Tanga Mjini, Innocent Omeme (35), na Abdul Aziz Nzori (31), wote wakazi wa Dar es Salaam.

Wengine ni Said Hassan (24), Rashid Hassan (23), Said Juma (30), Idd Kaniki (35), David Rupians (22), Salumu Salum (24), wote wakiwa ni wakazi wa Mkoani Dar es Salaam, Omary Mohamed (27), mkazi wa mkanyageni muheza, Tanga.

Kamanda Mwaibambe amesema, “Wamepangisha Nyumba nzima na tumewakuta na Vifaa mbalimbali ikiwamo majiko, laini za Simu, Simu aina mbalimbali pesa milioni 2,085,000 na karatasi ambazo zinakumbukumbu za majina ya Watu waliotapeliwa ambapo wanaweka alama ya vema ‘tiki’ kwa mtu aliyetapeliwa na laini husika huichoma moto.”

Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Julai 21, 2023
Fedha ya Fabinho kumshusha Palhinha Liverpool