Rapa 50 Cent ametangaza kujitoa rasmi kwenye mtandao wa Instagram unaomilikiwa na Facebook, akiweka picha inayomuonesha akiwa na kinywaji kusherehekea uamuzi wake.

Kiongozi huyo wa G-Unit aliyekuwa na wafuasi milioni 17.9, amesema kuwa amechukua uamuzi huo baada ya kuchukizwa na kitendo cha Instagram kuiondoa picha aliyoweka bila kumtaarifu.

“Ninaachana na IG, nirudi tena Twitter. Wanatoa vitu kwenye ukurasa wangu bila kunitaarifu,” ameandika 50 kwa lugha ya kiingereza yenye maneno makali.

Imeelezwa kuwa awali 50 aliweka picha ya inayoonesha imetolewa kwenye filamu ya ngono ya msanii Teairra Mari, picha ambayo hivi sasa haipo kwenye ukurasa wake baada ya kuondolewa.

Hata hivyo, mapema Jumatano wiki hii, Mari aliweka kwenye Instagram ujumbe akilaani kitendo cha mtu aliyedai alikuwa rafiki yake lakini aliweka kwenye Instagram picha yake ambayo ilipaswa kuwa ya faragha.

Kipengele cha pili cha mkataba wa Instagram kwa watumiaji kinasema: “Hautaweka picha za kihalifu, utupu, zinazobagua, zinazokiuka sheria, za chuki, za ngono au zenye ukakasi au nyingine zenye uelekeo huo.”

 

Facebook haijajibu chochote kuhusu uamuzi wa 50 Cent uliogeuka gumzo.

Mbunge Chadema acharuka Bungeni, amnyooshea kidole Mwijage
Fahamu makosa 5 yanayofanyika wakati wa kununua gari