Kufuatia agizo la Rais John Pombe Magufuli kusitisha michango ya fedha kwa wanafunzi walimu watatu wa shule ya msingi Nenge, akiwemo Afisa Elimu Kata ya Nyanguge mkoani Mwanza katika halmashauri ya Wilaya Magu, wamesimamishwa kazi kwa kukiuka agizo hilo.
Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Magu Lutengano Mwalwiba, amesema kuwa baada ya agizo la Rais Magufuli la kusitisha michango katika shule za msingi, Januari 23 mwaka huu aliwaonya wakuu wa shule na walimu wote, lakini Januari 24 waliendeleza kukusanya michango.
Mwalwiba meongeza kuwa watumishi hao wamekiuka mkataba wa elimu ya msingi bila malipo ambapo wamewachangisha shilingi 500 wanafunzi 378 wa shule hiyo kwa ajili ya nembo zautambulisho wa sare za wanafunzi kinyume na maagizo ya Rais Magufuli.
January 17 mwaka huu Rais John Pombe Magufuli alipiga marufuku michango kwenye shule za msingi na sekondari za serikali, na kuwaagiza Mawaziri Joyce Ndalichako na Waziri wa TAMISEMI Suleiman Jafo kusimamia agizo hilo.