Meneja wa klabu ya AC Milan, Gennaro Gattuso ameonyesha kuchukizwa na kiungo kutoka nchini Ufaransa, Tiemoue Bakayoko  aliyejiunga na klabu hiyo akitokea Chelsea kwa mkopo juma lililopita.

Gattuso alichukizwa na kiungo huyo, baada ya kushindwa kuwajibika ipasavyo katika mchezo wa mwishoni mwa juma lililopia (Jumamosi) uliowakutanisha na SSC Napoli na kujikuta wakipoteza kwa kufungwa mabao matatu kwa mawili.

Katika mchezo huo, Bakayoko alionyesha kiwango duni tofauti na alivyotarajiwa hali ambayo ilisababisha timu pinzani kumiliki eneo la kati na kusababisha kusawazisha mabao mawili kabla ya kuongeza la tatu.

Hadi dakika ya 50, AC Milan walikua akiongoza mabao mawili kwa sifuri, lakini udhaifu wa kiungo huyo wa kushindwa kuvuruga mipango ya SSC Napoli ulilkua chanzo cha timu yake kupoteza mchezo huo.

 

Mpango apangua laana za Makonda, 'Vitisho vya wanasiasa'
Rapa Swae Lee apasuliwa mdomo akiwa jukwaani