Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema kuwa changamoto ya upatikanaji wa ajira hususani kwa vijana imeanza kupungua nchini baada ya viwanda vingi kuanza kufanya kazi.

Amesema kuwa Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli imedhamiria kukuza uchumi kutoka wa chini hadi wa kati kupitia sekta ya viwanda ifikapo mwaka 2025.

Ameyasema hayo mara baada ya kutembelea kiwanda cha kukoboa kahawa cha BUKOP na cha kusindika kahawa cha Tanica, mjini Bukoba.

Aidha, amesema kwa sasa tabia ya vijana wengi kukaa vijiweni imepungua kwenye maeneo mengi nchini baada ya wengi kuajiliwa katika viwanda mbalimbali vilivyoanzishwa na kufufuliwa.

Majaliwa amesema viwanda vimekuwa vikitoa ajira nyingi kwa wananchi, ambapo alitolea mfano kiwanda kimoja cha Tanika kilichoajiri watumishi 800.

“Nyie mlioajiriwa kiwandani hapa hakikishe mnafanya kazi kwa bidii, weledi, uaminifu na uadilifu wa hali ya juu ili kukiwezesha kiwanda kuendelea na uzalishaji,” alisisitiza.

Hata hivyo, katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba.  Bernad Limbe kuhakikisha anatafuta eneo kwa ajili ya wafanyabiashara ndogo ndogo.

Breaking News: Mbunge Mwingine Chadema ajiuzulu na kuomba kuhamia CCM
Video: Dkt. Bashiru ahesabiwa siku CCM, Raia wawili wa China watimuliwa nchini