Nchini China wameanzisha shamba maalumu kwa ajili ya baishara ya ufugaji mende ambapo kwa mwaka shamba hilo linauwezo wa kutengeneza mende bilioni 6.
Mdudu huyu anauwezo wa kuishi muda mrefu bila kuwa na kichwa na hii ni kutokana na ubongo wake kupatikana tumboni na si kichwani kama ilivyo kwa wadudu na wenyama wengine.
Wanasayansi wanasema kuwa kulingana na tafiti zao mende wanauwezo wa kukaa muda mrefu maeneo yenye sumu na uchafu bila kudhurika, wamegundua kwamba huwa wanatoa kemikali zinazowasaidia kupambana na sumu.
Hivyo, Serikali ya China inaunga mkono kwa asilimia zote biashara ya ufugaji wa mende kutokana na mapato makubwa yanayoingizwa kutokana na biashara hiyo, kwani biashara hiyo inakadiriwa kuingiza Yuan bilioni 4.3 sawa na Trilioni moja na zaidi kwa pesa za kitanzania.
Aidha, Mende hao hutumika maalumu kwa kutibu baadhi ya magonjwa mbalimbali ikiwemo homa, malaria maumivu makali ya tumbo pamoja na mfumo wa hewa.
Na dawa hiyo tayari imeshatibu wagonjwa milioni 40 na zaidi katika hospitali 4,000.