Mkuu wa Mkoa wa Njombe ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama, Christopher Ole Sendeka amesema kuwa vyombo vya ulinzi na usalama vitawasaka popote walipo watekaji wa watoto watatu wa familia moja wanaodaiwa kutekwa January 20 na kusababisha taharuki kwa wakazi wa mkoa huo.

Ameyasema hayo wakati akizungumza na wananchi wa kijiji cha Ikando kata ya Kichiwa wilaya Njombe ambao wamekuwa wakiwatafuta watoto hao, ambapo amesema kuwa jeshi limejipanga vyema kuwabaini wahusika wa matukio ya utekaji na mauaji.

Kwa upande wake, Katibu wa hamasa wa chama cha mapinduzi mkoa wa Njombe, Johnson Mgimba amekiri kuumizwa kwa kiasi kikubwa na mikasa hiyo.

Kwa mujibu wa jeshi la polisi mkoani humo tayari watu wawili wanashikiliwa kwa kudaiwa kuhusika na matukio ya utekaji na mauaji ya watoto huku pia ikielezwa waganga ishirini wanahojiwa.

 

Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Januari 25, 2019
Monaco yamsimamisha kazi Thierry Henry